Showing posts with label Suala la GMO. Show all posts
Showing posts with label Suala la GMO. Show all posts

Friday, 7 September 2018

... KUUHARIBU UHAI WETU KUPITIA MIMEA ILIYOBATILISHWA KWA GMO- Sehemu ya pili



Juma lililopita tulifahamishana kuhusu GMO.
Kabla ya kuendelea tukumbushane hulka ya biashara hususan huku nchi zilizoendelea. Siku hizi ni kawaida  kabisa kwa wateja, Uzunguni, kutaka kujua nini wananunua, nini kitakachoingia tumboni, tarehe gani  bidhaa itaoza au kukosa thamani, nk. Wasiojali sana ni maskini au wasiosoma. Lakini hata hawa hulazimika kuchunguza  pale maradhi yanapobisha hodi. Tutoe mfano...
Uzunguni kuna tatizo kubwa la “allergies”
Allergies ni  nini?

WIMBI LA MIMEA INAYOBATILISHWA KWA GMO







Miaka sitini (hadi 100)  iliyopita-  sigara, ilivutia sana.
 Sinema na TV ziliionyesha waigizaji wakiivuta  mithili ya starehe ya hali ya juu sana. Nikiwa kijana tuliambiwa mwanamke alipovuta sigara kisha akampulizia mwanaume moshi usoni ni ishara ya kum-enzi, kumhitaji, kumtaka.
Sigara haikuonekana ni dhara.
Ila saratani ilipounganishwa na sigara- makampuni ya tumbaku yalichachamaa. Mvutano huu wa kibiashara ulichukua muda mrefu kupingika- hata mauaji na rushwa vilipita.
 Vitisho. Ufisadi.  Mabavu.