Monday, 24 December 2018

SINEMA ZA NGONO ZINAVYO ATHIRI VIJANA ULIMWENGUNI LEO-3Tuendelee na mada ya Jumapili mbili zilizopita.
Tumezungumzia sinema za ngono na namna zinavyohasidi afya na mahusiano ya watu. Sawa. Vipindi vya maisha yetu wanadamu hutofautiana. Kama ambavyo makala hii inakashifu sinema za ngono na changamoto zake ndivyo wazee wa miaka ile ya Sitini na Sabini walivyokasirishwa na suruali za vijana zilizotanuka chini (“Pekos”) , na sketi na magauni yaliyoishia mapajani (“Mini”).
 Linganisha na leo.  Vijana wanavalia suruali makalioni, kama wako maliwatoni  na wanawake wanaanika kabisa kila kitu mitandaoni au  maonesho.

SINEMA ZA NGONO ZINAVYO ATHIRI VIJANA ULIMWENGUNI LEO-2


Tuendelee na mada ya wiki jana.
Zamani sinema za ngono zilikatazwa kabisa na serikali ya Mwalimu Nyerere  na hata awamu zilizofuata. Leo zinaonekana waziwazi katika simu na wanawake kwa wanaume wanazikodolea macho. Matokeo kuna kudhalilishana pande zote mbili. Hii ni kutokana na taswira za waigizaji wachache wenye maungo yasiyofikana na hali halisi za wanadamu wengi.
Starehe hii kama zilivyo nyingi za kisasa zimeletwa na utandawazi na teknolojia za Kizungu. Sisi Waafrika hatukuwa na matatizo ya ngono au ufanyaji mapenzi. Mwalimu Nyerere na viongozi waliopita wallifahamu hilo ndiyo maana wakalikataza.
Miaka 30 hadi 50 iliyopita hatukuwa na matatizo ya mapenzi.

Nilipohamia Uzunguni nilishangazwa jinsi wenzetu walivyo na matatizo makubwa ya ngono.

SINEMA ZA NGONO ZINAVYO ATHIRI VIJANA ULIMWENGUNI LEO - 1

Wakati Mwalimu Nyerere akiwa Rais wetu, alisemwa vibaya, aliogopwa, alitaniwa. Ni ajabu namna leo, (nusu karne baadaye) anazungumziwa kwa staha, tija na hata kupendekezwa aitwe mtakatifu. Asiye na hatia au kosa. Sisi wanadamu wanafiki sana. Mtu akiwa nasi tunamsuta. Akishatutoka tunamvalisha kila suruali, viatu, bangili na kofia za jaha.
Nakumbuka tukiwa bado sekondari, tulisafiri sana Nairobi kutembea. Miaka hiyo ya Sabini Kenya ilifananishwa na Ulaya. Majuu. Nairobi  ilijaa klabu nzuri nzuri, mavazi ya Kizungu, sinema tele zikiwemo za ngono. Tuliwaona ndugu zetu wa Kenya wenye bahati sana.
Tulimsikia Rais wao, Jomo Kenyatta akisema: “Kuleni matunda ya Uhuru...”
Baadaye nilipokuwa mtu mzima, nikasafiri Ulaya. Kwa mara ya kwanza nikaona sinema ya ngono,  mwanzo hadi mwisho. Ilikuwa kioja. Sikuziona nikiwa shuleni, ( tuliposafiri Kenya) shauri ya masharti ya kiumri. Ziliitwa sinema za X. Yaani za watu wazima tu.

Sasa nikiwa Ughaibuni mtu mzima niliyeshapitisha miaka 25 sikuzuiwa. Niliufurahia uhondo uliokatazwa na Baba wa taifa na serikali ya TANU na CCM.
Lakini baada ya “kipya kinyemi” kwisha,  nikazoea, nikazikinahi. Nilianza kugundua watu walioangalia filamu hizo walikuwa wanaume wapweke wasiokuwa na wapenzi. Kila mtu alikaa peke yake, mle giza la sinema; akijishika shika; wengine wakinywa pombe kisirisiri. Kifupi waliotazama michezo hii walikuwa wapweke wenye matatizo ya kisaikolojia. Watu na wake zao hawakuhudhuria sinema za ngono. Ndiyo walikuwepo wapenzi walioziangalia. Mmoja mmoja na mkewe, lakini wachache...
Ziliitwa “pornography.”