Tuendelee na mada ya wiki
jana.
Zamani sinema za ngono
zilikatazwa kabisa na serikali ya Mwalimu Nyerere na hata awamu zilizofuata. Leo zinaonekana
waziwazi katika simu na wanawake kwa wanaume wanazikodolea macho. Matokeo kuna
kudhalilishana pande zote mbili. Hii ni kutokana na taswira za waigizaji
wachache wenye maungo yasiyofikana na hali halisi za wanadamu wengi.
Starehe hii kama zilivyo
nyingi za kisasa zimeletwa na utandawazi na teknolojia za Kizungu. Sisi
Waafrika hatukuwa na matatizo ya ngono au ufanyaji mapenzi. Mwalimu Nyerere na
viongozi waliopita wallifahamu hilo ndiyo maana wakalikataza.
Miaka 30 hadi 50 iliyopita
hatukuwa na matatizo ya mapenzi.
Nilipohamia Uzunguni nilishangazwa
jinsi wenzetu walivyo na matatizo makubwa ya ngono.
