Sunday 30 October 2016

KISWAHILI KINAVYOZIDI KUPARAGANYA HERUFI “R” NA “ L”





Watanzania tuamke jamani. Tumelala.
....Kiswahili kilianzia kwetu. Nchi kumi na moja zinazungumza lugha hii iliyotuunganisha na kutuletea amani zaidi ya miaka 100!
 Nchi kumi na moja! Ongezea idhaa kadhaa za redio, TV na mitandao jamii ughaibuni inayokitukuza Kiswahili. Jazia, vyuo.
 Hapa London kiko chuo maarufu cha lugha- SOAS ( School of Oriental and African Studies- Shule ya Masomo ya Mashariki na Afrika).

Wednesday 12 October 2016

OF HORNETS, SPIDERS AND A SMASHED CAR WINDOW

If we start today’s chat with the word Vespinae, would you, instantly,  get what I am talking about? It would be wrong to suppose it is reference to the small motorbike called Vespa. Sorry, no pun intended but, Vespa is a joke compared to what Vespinae actually means. That dear friends, is the scientific name of Nyigu or Manyigu in Kiswahili. The no -nonsense insect bit me when I was a child growing on the slopes of Mount Kilimanjaro. I might have been eight or nine AND funnily, I still remember the pain. Vividly. Like it was five minutes ago. So intense that I should compare the experience to a bullet wound; which not many of would like to try out, nor imagine.

VIPI TATIZO LA FIGO LAZIDI KUATHIRI AFYA ZA WAAFRIKA?- Sehemu ya 2




Majuma matatu yaliyopita safu hii ilizungumzia  tatizo la maradhi ya figo. Punde tu wasomaji kadhaa waliniandikia kuulizia habari zaidi.
Takwimu za afya Ulaya zinasema figo huandama zaidi watu weusi.
Ingawa bara lina kila aina ya virutubisho , mazao na hali ya hewa safi, bado hatujijali kiafya.
Je maradhi ya figo yanaepukika? Na kuanzia, figo ziko wapi na kazi yake ni nini?
Figo mbili ziko , juu ya nyonga,  chini ya ubavu, mgongoni. Kawaida mabondia wanapodundana, wakikaribiana, kila mmoja hujaribu kupiga figo. Kwanini figo idundwe?

VIPI TATIZO LA FIGO LAZIDI KUATHIRI AFYA ZA WAAFRIKA? - Sehemu 1



Tiba na afya za dunia yetu zimegawanyika sehemu mbili kuu.
 Magharibi ni uganga wa Kizungu unaotumia sayansi iliyofikia kilele karne ya 19 na 20. Moja ya nguzo zake kuu ni kutibu kwa kunyamazisha- kupitia sindano, dawa na upasuaji. Tiba ya Kizungu ndiyo inayotawala dunia yetu na ndiyo mara nyingi Wabongo wanaojiweza wakiugua siku hizi husafrishwa nje  kutibiwa.
Tiba za mashariki zinaongozwa na ustaarabu wa Kihindi na Kichina. Wahindi hutumia mwenendo uitwao Ayurveda. Tiba hii yenye zaidi ya miaka elfu mbili huangalia mwili mzima ukoje kabla ya kuushughulikia. Wachina wanao pia mtindo huo huo, unaotazama mtiririko wa nguvu mwilini badala ya dosari. Utaratibu wa Kichina na Kihindi kijumla hautibu tatizo moja kama  Wakizungu. Kwa wazungu mathalani ukiumwa kichwa utapewa dawa ya kuyaondoa maumivu hayo.

Tuesday 4 October 2016

WASANII WAKAZI UINGEREZA WAJIUNGA CHINI YA BALOZI MIGIRO



 Moja ya mambo yanayochekesha na kusitikitisha kuhusu Watanzania wakazi Ughaibuni ni kuogopana. Si tu kuogopana kama ilivyo  Afrika nzima, yaani hofu ya kulogana. Wala si tu  kuwa na wasiwasi wa fitina na masengenyo ya eti mwenzako atakujua unakulaje, unalalaje au utawezaje  kumsaidia.
Hofu ya kukwepa ofisi zetu za Ubalozi.