Habari zilizotanda Uingereza majuma mawili yaliyopita zimehusu gazeti maarufu la News Of The World. Lilifungwa wiki jana baada ya mashtaka ya uhalifu. News of the World ilikuwa ikipata habari kwa kuingilia barua pepe na simu za watu maarufu ili kuwaiba. Miongoni mwa waliokuwa wakifanyiwa wizi huo ni Malkia Elisabeth, mwanae Prince Charles, Waziri Mkuu wa zamani Gordon Brown, viongozi mbalimbali na wacheza mpira mashuhuri. Mwishoni gazeti liliwaudhi wananchi zaidi ilipofahamika lilikuwa limekita makucha yake kusikiliza habari za watu waliouliwa au kufa. Kati yao ni wasichana watatu waliouliwa kinyama Milly Dowler, Jessica Chapman, Holly Wells na ndugu za waliofariki Julai 2005 kutokana na mabomu ya magaidi mjini London.
Suala la kutafuta habari hata za maiti lilikuwa kilele cha uhalifu na gazeti lilifungwa na mwenyekiti wake Rupert Murdoch.
Mzee Murdoch na mkewe mzawa wa China,Wendi Deng, aliyezaliwa mwaka 1968...
Picha ya Gettys...
<--more--!>