Je, pana faida gani kusikiliza habari za Mmarekani mweusi Gil Scott- Heron aliyefariki mwezi uliopita? Sidhani wapo Watanzania wengi seuze Waafrika waliomjua msanii huyu aliyetoa albam 15 za muziki na vitabu vitano; vitatu vya mashairi na riwaya mbili alizochapa akiwa bado shuleni. Gil Scott- Heron alipofariki Ijumaa Mei 27 akiwa na umri wa miaka 62, alibeba taji la mwasisi wa muziki wa Hip Hop na “Bob Dylan Mweusi.”
Gil Scott-Heron akitumbuiza na bendi yake "Amnesia Express" ukumbi wa Jazz Cafe, London mwaka 1999. Picha na F Macha <--more--!>