Hali ngumu ya uchumi na maendeleo imezusha vijana wengi wasio na kazi; wanaranda randa ovyo barabarani, wakitega na kusogoa vijiweni, wakijaribu hili na lile. Watoto yatima hawana wazazi kutokana na maafa ya maradhi ya Ukimwi na jamii yetu inazidi kukuuza wananchi wasiokuwa na matumaini. Yote haya yanaweza kumea hasira, kero na ghasia tupu.
Miezi michache Mickey Mikidadi Jones alikuwa likizo nyumbani. Hali ilimkuna sana.
Leo Mickey Mikidadi Jones, kaamua kujihusisha na mtandao wa kuwaunganisha vijana wa ughaibuni na kwetu Bongo kuboresha maisha yao. Mara nyingi nilipomhoji Mickey alimtupia maswali dada Lydia Mkude, ambaye ni mshauri mkuu wa MMVT ("Mtandao wa Maendeleo ya Vijana Tanzania").
Solomon Gaddi (mwenyekiti wa MMVT) akihutubia kikao. Kushoto kwake ni Haruna Mbeya (mwakilishi , Ughaibuni) na mwanzo kabisa Mshauri na mwakilishi wao wa kimataifa mtandaoni, Mickey Mikidadi Jones. Picha ihsani ya MMVT.
<--more--!>