Uandishi wa mablogu wahitaji tarakilishi. Tarakilishi ni neno fasaha la Kiswahili linaloimanisha Kompyuta. Na hiki si chombo tu cha kuandikia. Huendesha simu za mkononi; taa zinazoongoza magari barabarani, mitambo ya ndege, mahospitali, runinga, nk. Dunia ya leo inaongozwa na tarakilishi. Hili ni bado somo jipya Tanzania. Kidunia mtandao kama tunavyoujua una miaka 15 ingawa sayansi hii ya kihabari imekuwepo kwa takribani miaka 30. Awali ilitumiwa na watu wachache hasa wanajeshi na majasusi kulinda matakwa ya serikali mbalimbali.
Rosemary Mizizi, blog lake Mwanamke na Nyumba linazungumzia mahusiano nyeti kati ya wanawake na wanaume kwa undani sana katika jamii ya Tanzania leo.
<--more--!>