Showing posts with label Ukoloni na Dini. Show all posts
Showing posts with label Ukoloni na Dini. Show all posts

Thursday, 13 December 2012

NINI MIZIZI YA TATIZO LA WAISLAMU KUCHOMA MAKANISA NA AMANI AFRIKA?-Sehemu ya 2


 Jumapili iliyopita tuliona namna mwanamuziki Fela Kuti  alivyoonya kuhusu imani za kigeni zilivyochangia kupotosha utamaduni wa Mwafrika.
Akasisitiza : “Ukristo na Uislamu si dini zetu...Wakristo wana fikra na tabia  za Waingereza na Wamarekani, ilhali Waislamu wana tabia za Waarabu.” 
 Msikilize mwenyewe akijieleza kinaga naga
Jadi mbalimbali duniani  zilijengwa kufuatana na mazingira na hali ya hewa. Dini zilitumia mvua, jua, radi, miti, wanyama nk,  kuabudu na kutambika.  Dini mbili kuu za Waafrika leo zimetokana na utamaduni wa Mashariki ya Kati na Wazungu.


<--more--!>

NINI MSINGI WA TATIZO LA WAISLAMU WANAOHARIBU MAKANISA NA AMANI AFRIKA? -Sehem ya 1


Sijui wasomaji wangapi tunamkumbuka mwanamuziki mashuhuri wa Nigeria, Fela Anikulapo Kuti aliyefariki 1997 akiwa na umri wa miaka 59?  Fela alikuwa binam wa mwandishi maarufu, Wole Soyinka (pichani) aliyeshinda tuzo la fasihi (Nobel) duniani 1986.

Pamoja na kipaji cha muziki (utunzi wenye ujumbe mzito, kuimba, kupiga saxafoni, ngoma na piano) Fela hakua mwoga.  Alikuwa mmoja wa wanamuziki wachache Afrika ambaye hakusita si tu kuimba ukweli, bali tayari kupambana na serikali ya nchi yake na kukemea ufisadi na rushwa vilivyoinyea(na bado vinaendelea) Nigeria.

Serikali na majeshi yalimchukia na kumwandama kiasi ambacho mwaka 1977 askari elfu moja walivamia makao makuu ya bendi yake -Afrika 70-  wakampiga yeye, wake zake na wanabendi halafu  wakaharibu kila kitu. Ndani ya vurugu hiyo walimtupa mamake Fela (Funmilayo) dirishani – baadaye akafia hospitalini. Fela aliudhika sana akatunga  nyimbo mbili kuishutumu serikali na askari wadhalimu (“Coffin for Head of State” na “Unknown Soldier”) na kulipeleka jeneza la mama mzazi makao makuu ya jeshi yaliyoongozwa na Jenerali Olusegun Obasanjo(aliyekuja kuwa Rais). Licha ya kipigo,  baadaye alitafutiwa vijisababu akafungwa jela miaka mitano kwa msimamo usiokua na woga wala unafiki.
Tuangalie dhana ya unafiki.
Fela Kuti alioa wake 27 (aliowaita malkia ), mwaka 1977;  waliimba na kucheza naye jukwaani.  
<--more--!>