Karibuni
rafiki yangu Mzungu alikuwa Afrika.
Taaluma
yake ni uanahabari. Anaipenda sana
Afrika na watu wake. Zamani babu aliishi India na alipinga sana ukoloni. Ana
mke na watoto wawili. Shughuli zake
humzungusha kila sehemu. Analijua bara
kuliko hata tuliozaliwa huko. Baada
ya sifa na vicheko, ghafla alisuta
mapenzi.
“Ningekuwa
mmoja wa babu zenu zamani Bwana Freddy ningenyaka wake ishirini. Kila nilikokwenda sikukosa sahiba. Wanataka niwatumie tikiti za ndege. Waje Ulaya
waishi raha mustarehe. Ni vigumu sana kuwahimiza dada hawa kwamba maisha yangu
si ya kitajiri. Hata ningekuwa tajiri kwetu Ulaya ndoa za mitala haziruhusiwi. Na mke wangu hatofurahi akisikia nina wake
wengine!”
Inachekesha
alivyosema, lakini ndiyo kichuguu cha mchwa hicho.
