Showing posts with label Abert Mangwea. Show all posts
Showing posts with label Abert Mangwea. Show all posts

Monday, 17 June 2013

KIFO CHA ALBERT MANGWEA – KINATUULIZA MASWALI GANI- Sehemu ya Pili



Kwanza kabla ya kuendelea na (kumalizia) mada tuliyoianza wiki jana,  tuwape pole ndugu wa familia yake Albert Mangwea. Tuwape pia pole marafiki zake na wote waliomjua kwa karibu. Tuwaombe radhi kwa kuendelea kuzungumzia jambo ambalo linawakumbusha uchungu wa mtu aliyekwisha zikwa.
Pamoja na hayo tujikumbushe madhumuni ya kuandika na kuzungumzia suala hili.
Kwanza kabisa kupoteza vijana wanaoanza maisha katika hali hizi mbaya si jambo zuri. Wapo wengi wanaondelea kuzungumzia kwamba ni Mungu kaamua na kwamba kifo ni asili maisha. Hatukatai hilo. Ila kwetu Tanzania imekua sasa desturi kukubali vifo na utamaduni wa kufa mapema.  Wanapoendelea kufariki vijana tunakubali ni maajaliwa. Zikitokea ajali za magari (zinazouzilika) zilizotokana na uzembe  wa madereva pia tunalitaja jina la Mungu. Mungu amekuwa sasa ndiye  mwamba wa kila baya. Kageuka kisingizio. Kwanini sisi tu ndiyo kitakwimu tuna vifo vingi zaidi tena vya watu wenye umri mdogo?
Lakini kabla ya kuendelea zaidi, tukubaliane ...

KIFO CHA ALBERT MWANGEA -KINATUULIZA MASWALI GANI?- Sehemu 1



Babu wa fasihi ya Kiswahili, Shaaban Robert alifariki mwezi huu  mwaka 1962. Ingetakiwa sikukuu ya kifo  chake yaani Juni 20  ifanyiwe maadhimisho kila mwaka. Sisi na wenzangu wa bendi ya Sayari tuliwahi kusheherekea kwa maonyesho ya 1983. Hazina hii tukufu ya taifa inatakiwa zaidi ya hilo.
  Moja ya vitabu vyake babu ni  “Kielezo cha Fasili” (kilitolewa upya na mwongozi wa wachapishaji Tanzania; “Mkuki na Nyota” ,2004) kinafafanua mashairi yake kwa wasomaji mintaarafu  ya kujenga mapafu kilugha.
Ananyambua  Shairi la “Jina”: “Mwanadamu mwenye fikra njema huacha fahari au sifa kwa watu ambayo vizazi vyake vya nyuma yake hupenda kuiona, na ambayo itakuwa kama hazina kwa watu wote katika dunia.”
Albert Mangwea hakua Shaaban Robert;  kafa akiwa na miaka 31 tu. Lakini  Mangwea au Mangair alitumia fani ya ushairi kuchangia kuiendeleza fasihi ya Kiswahili  na kipaji chake alichomegewa na Muumba.
Kifo  hiki kilichokua Usauzi (Afrika Kusini) kimeongelewa na kinaendelea kuongelewa. Mwaka jana wakati huu Tanzania ilimpoteza Steve Kanumba. Vifo vya chipukizi hawa vimeacha utata na mijadala marefu.
 Mangwea alifia ughaibuni.  Maisha ugenini ni magumu maana habari huwa hazitangazwi sana. Mbali na taratibu za kisheria na itikeli, kinachongojewa kutufariji huwa viongozi wa dini na serikali.