Showing posts with label Dawa na Maradhi yetu. Show all posts
Showing posts with label Dawa na Maradhi yetu. Show all posts

Sunday, 21 April 2013

TATIZO KUBWA LA VIRUSI SUGU LEO LIMETOKANA NA UTOAJI DAWA KALI KIHOLELA...


Enzi hizo hatukua na UKIMWI.
Magonjwa ya zinaa hayakuua mtu. Dalili yake ilikuwa kuwashwa na kujisikia vibaya wakati wa kwenda haja ndogo tu, basi.  Yakikuzidia  unazunguka zunguka mitaani unanunua dawa  rangi ya chungwa na manjano- kidonge cha “tetracylene”- aghali ndiyo; lakini kinamaliza kabisa tatizo.
Baadaye miaka ya Themanini UKIMWI ukatangaza ufalme.
UKIMWI haukuponywa kwa kidonge kama hicho.

 Na hata baada ya miaka thelathini, UKIMWI uliposhaanza kutibika- ( nchi zilizoendelea), haikua kidonge kimoja. Vingi.  Tena bei yake si ya porojo. Sijasikia mtu anayeweza kuingia tu sehemu akanunua msururu wa vidonge vya kutibu UKIMWI. Tiba hii ilihimili lakini haijaondoa kirusi, abadan.