Moja ya mambo yanayochekesha
na kusitikitisha kuhusu Watanzania wakazi Ughaibuni ni kuogopana. Si tu
kuogopana kama ilivyo Afrika nzima,
yaani hofu ya kulogana. Wala si tu kuwa
na wasiwasi wa fitina na masengenyo ya eti mwenzako atakujua unakulaje,
unalalaje au utawezaje kumsaidia.
Hofu ya kukwepa ofisi zetu
za Ubalozi.


