Kwanza nakutakia kheri za mwaka mpya wa 2016.
Ninakupongeza kwa
kuanza kazi yako kwa kishindo. Kishindo kinachowapa wananchi wetu matumaini.
Mvumo unaoukupa sifa Afrika Mashariki nzima hadi kuwafanya wenzetu watuonee
wivu. Afrika nzima inatamani ingekuwa na
viongozi kama wewe. Tunaoishi Ughaibuni tutaendelea kuwa mabalozi wako.
Leo mada yangu Mheshimiwa Rais ni suala la ukeketaji.
Wasichana waliokimbia kujihifadhi jumba la Mugumu, Mara. Picha ya Anthony Mayunga kupitia gazeti la Mwananchi.


