Tupo sebuleni kwa jirani yangu mmoja
mwanamke. Katualika majirani kusherehekea siku ya kuzaliwa miaka themanini. Themanini
nakwambia! Wanawe wawili wamewasili na wajukuu na vitukuu toka Australia na
Afrika Kusini kushangilia siku hii maalum ya ajuza mcheshi, roho safi; kibibi
anayependwa na kila mtu hapa mtaani ninapoishi London.
Mama wa Kizungu na mwanae wakingojea kuvuka barabara kando ya basi la ghorofa London...picha na F Macha...
Nyumba imetota baraka. Harufu mbalimbali za makulaji zinazitesa pua.
Vyakula vimetandazwa mezani. Viazi Ulaya
vya kuchemsha na kuoka vinavyotengeneza msosi maarufu uliovum buliwa na hawa
hawa Waingereza unaojulikana kama Chips. Mboga mbichi safi za saladi, nyanya,
matango, vitunguu, jibini (chizi), mikate ya kila sampuli, samaki na kuku wa kukaanga. Kawaida karamu za Majuu
hutenganisha walaji wa nyama na wasiokula nyama (Vegetarians).
<--more--!>