Dunia yetu ina kila aina za udongo.
Udongo wa Mpirani nje kidogo ya Moshi mjini unanikumbusha wa Kigoma ambapo rangi yake inakurubia wekundu. Mimea ya Mpirani ni migomba, mapera, machungwa, ndimu, maembe, kahawa na gari analoendesha dada yangu Juliana linakwenda taratibu, likikwepa mashimo shimo ya udongo huu.
“Unaona ule msikiti?” naulizwa. Nikiwa mdogo haikuwepo misikiti mashambani Moshi. Kidesturi migombani kwa Wachagga hujazana makanisa.
“Wapo mangi wengi Waislamu siku hizi,” dereva anafafanua.
<--more--!>