Habari kuhusu tiba ya Loliondo zimezigusa hisia za Watanzania wengi. Huku nje suala la mzee Mchungaji Ambilikile Mwasapile; halijafahamika vizuri. Wanahabari wachache tumefuatilia mambo ya “mti wa Loliondo” mitandaoni lakini si jambo la jazba kama nyumbani. Suala lolote linalowasaidia wanadamu kuondokana na matatizo yao ya kimaisha huwa na umuhimu katika jamii. Loliondo imewika kutokana na afya zetu kuzidi kuwa mbaya.
Waafrika tunatafuta majibu ya haraka.
Waingereza hutumia neno “Quick Fix” kuelezea ufafanuzi wa kupinda kona. Wabrazili husema “um jeitinho” (tamka, jeichinyo) kufumbua matatizo upesi upesi. Ni kama mtu huna hela ya chai ukala kiporo. Wachagga tuna chakula kinaitwa “Ikato” (mseto wa maharage na ndizi); badala ya mkate au maandazi.
<--more!-->